Kongamano Kuelekea Maadhimisho Ya Siku Ya Utalii Duniani

Chuo Cha Uhasibu Arusha IAA kwa kushirikiana na Rethinking Tourism Africa wameandaa kongamano lililohusisha wadau wa sekta ya utalii katika kuelekea siku ya utalii duniani lililofanyika katika Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha.

Akifungua kongamano hilo Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti, na Ushauri wa Kitaalam Prof. Epaphra Manamba kwa niaba ya Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) amesema utalii ni moja kati ya sekta muhimu ambayo inamchango mkubwa katika kuleta maendeleo nchini Tanzania.

Aidha Prof. Manamba ameongeza kuwa sekta ya utalii imeendelea kukuwa kwa kasi na kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi, na hii ni kutokana na juhudi anazozifanya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hivyo ni vyema watanzania wote wakamuunga mkono katika uhifadhi wa vivutio vya utalii hapa nchini.

Kongamano hilo limefanyika leo tarehe 26 septemba 2023 na kuudhuriwa na wakufunzi kutoka katika vyuo vinavyotoa kozi za utalii, wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii.